Maria kutolewa hekaluni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Bikira Maria Kutolewa Hekaluni ni kumbukumbu ya liturujia inayoadhimishwa na Wakatoliki na Waorthodoksi tarehe 21 Novemba[1][2].

Msingi
Adhimisho linatokana na habari ambayo haipatikani katika Agano Jipya, ila katika Injili ya Yakobo. Humo inasimuliwa kwamba wazazi wa Bikira Maria, Yohakimu na Ana, ambao hawakuwa na watoto, walipata ujumbe kutoka mbinguni kwamba watapata mtoto.
Kama shukrani ya kupata mtoto wa kike, akiwa bado mdogo walimleta katika Hekalu la Yerusalemu ili kumweka wakfu kwa Mungu[3].
Huko alibaki hadi alipotolewa kwa Yosefu.[3][4]
Kwa namna nyingine, inaaminika kwamba mwenyewe alijitoa mapema kwa Mwenyezi Mungu, yeye aliyejaa neema tangu kutungwa mimba kwa kukingiwa dhambi ya asili na atakayejaliwa kuwa Mama wa Mungu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu [5].
Remove ads
Asili
Sikukuu ilianzishwa kuhusiana na kutabaruku Basilika jipya la Mtakatifu Maria, lililojengwa mwaka 543 na kaisari Justinian I karibu na mabaki ya Hekalu la Yerusalemu.[4]
Kutoka Ukristo wa mashariki sikukuu ilienea katika monasteri za Italia Kusini katika karne ya 9, ikaingia katika liturujia ya Papa wa Avignon mwaka 1372 kwa agizo la Papa Gregori XI.[6][7]
Picha
- Mchoro wa Bartolo di Fredi, 1360 hivi.
- Mchoro mdogo wa Limbourg Brothers, 1415 hivi.
- Mchoro wa Sano di Pietro, 1450 hivi.
- Mchoro wa Fra Carnevale, 1467 hivi.
- Mchoro wa Master of Wilten, karne ya 15.
- Mchoro wa Hans Holbein the Elder, 1493.
- Mchoro wa Cima da Conegliano circa 1500.
- Mchoro wa Titian, 1535 hivi.
- Picha takatifu ya Russia, karne ya 16.
- Mchoro wa Alfonso Boschi, karne ya 17.
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads