Stefano Vinh

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Stefano Vinh (1813-1839) alikuwa mkulima wa Vietnam aliyekuwa mkatekumeni bado, ambaye, kwa kukataa kukashfu msalaba, alifungwa, akateswa, akanyongwa kwa amri ya kaisari Minh Mang.

Pamoja naye walipatwa na mambo hayohayo makatekista Fransisko Ha Thong Mau na Dominiko Buy Van Uy, mshonaji Thomas Nguyen Van De, na mkulima mwenzake Augustino Nguyen Van Moi aliyekuwa amebatizwa tangu muda mfupi [1].

Ni kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (16251886).

Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.

Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 19 Desemba[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads