Thomas De Van Nguyen
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Thomas De Van Nguyen (1811-1839) alikuwa mshonaji wa Vietnam ambaye, kwa kukataa kukashfu msalaba, alifungwa, akateswa, akanyongwa kwa amri ya kaisari Minh Mang.
Pamoja naye walipatwa na mambo hayohayo makatekista Fransisko Ha Thong Mau na Dominiko Buy Van Uy, mkulima Augustino Nguyen Van Moi aliyekuwa amebatizwa tangu muda mfupi, na mkulima mwenzake Stefano Nguyen Van Vinh aliyekuwa mkatekumeni bado [1].
Ni kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886).
Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 19 Desemba[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads