The Documentary
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
The Documentary ni albamu ya kwanza kutolewa na rapa wa West Coast - The Game. Albamu ilitolewa mnamo tarehe 18 Januari 2005 kupitia studio ya Interscope Records. Ni baada ya kupata afadhali ya majelaha yake aliopigwa na risasi kunako mwishoni mwa mwaka wa 2001, The Game akajiendeleza na maswala yake ya kurap na akaja kugunduliwa na Dr. Dre, ambaye baadaye alimsajiri katika stuido yake ya Aftermath Entertainment.
Utayarishaji wa albamu hiyo haukuwekewa vizingiti kuwa Dr. Dre ndiye atakaye tayarisha tu, bali hata Kanye West na Timbaland nao walitia mikono yao, na kwa upande wa waimbaji alikuwemo 50 Cent, Nate Dogg, na Faith Evans
Albamu ya The Documentary imepata kutajwa kuwa ni albamu namba moja katika albamu 200 bora katika mauzo ya Billboard, kufikisha kiwango cha kuuza nakala 586,000 katika wiki ya kwanza. Na kuifanya albamu kupata platinamu mara mbili katika mwezi wa Machi mnamo mwaka wa 2005 na pia kuweza kuuza zaidi ya nakala milioni sita kwa hesabu ya dunia nzima.
Remove ads
Orodha ya nyimbo
Maelezo kuhusu albamu ya The Documentary yamechukuliwa kutoka katika 's marejeo ya albamu hii.[1]
Remove ads
Chati
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads