Tundu Antiphas Mughwai Lissu
Mwanasheria, Mwanasiasa, Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Raisi wa Tanganyika Law Society (TLS) From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Tundu Lissu (jina la kuzaliwa Tundu Antiphas Mughwai Lissu; alizaliwa mkoani Singida, 20 Januari 1968) ni mwanasiasa, wakili, na mbunge wa zamani wa Tanzania ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti [1] wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nchini Tanzania. Anajulikana kwa msimamo wake wa wazi dhidi ya rushwa, ukiukwaji wa haki za binadamu, na matumizi mabaya ya madaraka. Lissu aliwahi kuwa Mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama cha upinzani cha Chadema na pia alikuwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho. Ametambulika kwa ukosoaji wake mkali dhidi ya serikali, hali iliyomfanya kuwa mmoja wa wanasiasa mashuhuri na wenye ushawishi mkubwa katika siasa za upinzani nchini.[2]

Mnamo Septemba 2017, Lissu alinusurika jaribio la mauaji baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 16 mjini Dodoma — tukio lililoibua maswali mengi kuhusu usalama wa wanasiasa wa upinzani. Baada ya matibabu ya muda mrefu nchini Kenya na baadaye Ubelgiji, Lissu alirejea Tanzania mwaka 2020 na kugombea urais kupitia Chadema, ingawa hakushinda. Licha ya changamoto alizokumbana nazo, bado anahesabiwa kuwa sauti muhimu katika harakati za kudai demokrasia, utawala wa sheria, na haki za kiraia nchini Tanzania.
Remove ads
Maisha
Tundu Lissu alizaliwa na wakulima. Alisoma Shule ya Sekondari Ilboru ya Arusha na kuhitimu mwaka 1983, halafu alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.[3]
Alichaguliwa kuendelea kuwa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi wa mwaka 2015.[4]
Tungu Lissu husifika kwa tabia yake kuikosoa serikali kwa kiasi kikubwa akitumia taarifa na takwimu nyingi. Kumekuwa na matatizo chungunzima yaliyowekwa wazi na mbunge huyu na alishawahi kusema hatanyamaza kuikosoa serikali, labda afe.
Alisema hivyo kwa sababu mara kadhaa alikamatwa na polisi na kutiwa ndani hadi alipokubaliwa kuweka dhamana.
Mnamo tarehe 7 Septemba 2017 majira ya saa saba mchana alipigwa risasi 38, lakini 16 tu katika hizo ndizo zilizompata katika sehemu za mkononi, miguuni na tumboni.[5][6] Tukio hilo lilitokea nyumbani kwake Dodoma Area D. Baada ya kupata matibabu ya awali, Lissu alisafirishwa hadi jijini Nairobi kwa matibabu zaidi.[7]
Baada ya hapo alisafirishwa hadi Ubelgiji alipoendelea kufanyiwa upasuaji hadi kufikia operesheni 22.
Tukio hili limelaaniwa vikali na viongozi na watu mashuhuri mbalimbali nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na Rais John Magufuli aliyeandika kwa masikitiko katika ukurasa wake wa Twitter kwa kulaani tendo hilo lisilo la kibinadamu.[8]
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anayetambuliwa na vyombo vya dola, Profesa Ibrahim Lipumba, naye ameonesha kukerwa na tukio la kutandikwa risasi kwa Lissu. Kwa uchungu, Lipumba amevitaka vyombo vya dola kuwatafuta wahusika wa tukio na wapelekwe katika vyombo vya sheria mara moja.[9]
Hata hivyo, hakuna mtu aliyekamatwa kutokana na upelelezi.
Lissu alikaa Ubelgiji kwa mayibabu lakini pia kwa wasiwasi kuhusu usalama wake nchini Tanzania hadi mwaka 2020 alirudi kwenye mwishoni mwa Julai ili agombee urais.
Mnamo Januari 2023, Tundu Lissu alitangaza kuwa amerejea Tanzania baada ya miaka mitano ya uhamishoni nchini Ubelgiji.[10]
Mnamo Januari 2025, Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kimemchagua Tundu Lissu kuwa kiongozi mpya kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025, wakati ambapo kinakabiliwa na ongezeko la ukandamizaji wa kisiasa.[11]
Aprili 9, 2025, Lissu alikamatwa kwa tuhuma ya uhaini baada ya kudai mageuzi katika taratibu za uchaguzi mkuu ujao katika mkutano wa hadhara mjini Mbinga.[12]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads