Upietisti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Upietisti (kwa Kiingereza Pietism, kutoka neno la Kilatini pietas, yaani heshima kwa Mungu, kwa wazazi, kwa ndugu na kwa nchi asili) ulikuwa tapo lenye athari kubwa kati ya Walutheri, lakini pia kwa madhehebu mengine ya Uprotestanti, na hata kwa Wakatoliki huko Ulaya na Amerika Kaskazini[1] tangu mwishoni mwa karne ya 17.

Uliunganisha mikazo ya Kilutheri kuhusu mafundisho ya Biblia ya Kikristo na mikazo ya Kikalvini kuhusu maadili imara.
Remove ads
Historia
Asili yake ni Ujerumani ya leo na kazi ya Philipp Jakob Spener, mwanateolojia Mlutheri aliyesisitiza mabadiliko ya Mkristo kwa aina ya kuzaliwa upya. Ingawa yeye hakudai wafuasi wake wajitenge na Wakristo wenzao, mahimizo yake yalielekea huko.
Upietisti ulienea kwanza Uswisi na nchi nyingine za lugha ya Kijerumani barani Ulaya, halafu Skandinavia na Baltiki (ulipoathiri zaidi tena utamaduni wa Kikristo kupitia watu kama Hans Nielsen Hauge huko Norway, Carl Olof Rosenius huko Sweden, Katarina Asplund huko Finland na Barbara von Krüdener katika nchi za Baltiki), na hatimaye Ulaya nzima.
Kutoka huko ulipelekwa Amerika Kaskazini, hasa kwa njia ya wahamiaji kutoka Ujerumani na Skandinavia, ukaathiri Waprotestanti wenye asili tofauti ukachangia katika karne ya 18 mwanzo wa Ukristo wa Kiinjilisti, ambao leo una waumini milioni mia tatu.
Tapo la Upietisti ndani ya Ulutheri lilifikia kilele chake katikati ya karne ya 18, lilififia kati karne ya 19 na kutoweka Amerika mwishoni mwa karne ya 20.
Hata hivyo, baadhi ya misimamo yake iliathiri Uprotestanti kwa jumla, ikimchochea kasisi Mwanglikana John Wesley kuanzisha tapo la Wamethodisti, na vilevile Alexander Mack kuanzisha tapo la Schwarzenau Brethren kati ya Waanabaptisti.
Huko Marekani, Upietisti ulitawala pia kati ya Quakers, Wakalvini, Wabaptisti, Waanglikana n.k.
Remove ads
Tazama pia
- Amana Colonies
- Adolf Köberle
- Barbara Juliana von Krüdener
- Carl Olof Rosenius
- Erik Pontoppidan
- Friedrich Christoph Oetinger
- Friedrich Hölderlin
- Johann Georg Rapp
- Hans Adolph Brorson
- Hans Nielsen Hauge
- Haugean
- Johann Georg Hamann
- Harmony Society
- Henric Schartau
- Immanuel Kant
- Johann Albrecht Bengel
- Johann Conrad Dippel
- Johannes Kelpius
- Kanisa la Ndugu
- Kanisa la Moravian
- Katarina Asplund
- Philipp Jakob Spener
- Theologia Germanica
- Nicolaus Ludwig von Zinzendorf
- Wakarismatiki
- Wamethodisti
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads