Ushetu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ushetu ni kata iliyo makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu katika Mkoa wa Shinyanga, Tanzania. Eneo hili linapatikana kilomita 52 kusini mwa mji wa Kahama.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 25,471 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 17,538 waishio humo.[2]
Kuna jamii mbili ambazo ni asilimia kubwa ya watu wanaoishi humo: Wanyamwezi na Wasukuma.
Mazao ya biashara yanayolimwa katika eneo hili ni pamba na tumbaku, huku mazao ya chakula yakiwa ni mahindi, mpunga, karanga, maharage, viazi vitamu na mazao mengine madogomadogo.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads