Vendemiale

From Wikipedia, the free encyclopedia

Vendemiale
Remove ads

Vendemiale (alifariki 483) alikuwa askofu wa Gafsa (leo nchini Tunisia) hadi alipopelekwa uhamishoni katika kisiwa cha Corsica (leo nchini Ufaransa) kutokana na dhuluma za Wavandali Waario dhidi ya Wakatoliki. Ilikuwa vilevile kwa maaskofu wengine 650.

Thumb
Mt. Vendemiale katika dirisha la kioo cha rangi.

Baada ya kuinjilisha kisiwa hicho pamoja na maaskofu Eujeni wa Karthago na Lonjino wa Pamaria, aliendelea hata nje yake. Hatimaye alifia dini kwa kukatwa kichwa kwa amri ya mfalme Huneriki [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Mei[2][3].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads