Vitus Bering

From Wikipedia, the free encyclopedia

Vitus Bering
Remove ads

Vitus Jonassen Bering (aliitwa pia jina la Kirusi: Ivan Ivanovich Bering; 1681 - 1741[1]) [2] alikuwa baharia na mpelelezi kutoka nchini Denmark aliyejiunga na jeshi la majini la Urusi mnamo mwaka 1704. Wakati wa Vita Vikuu vya Kaskazini alijipatia sifa na kupandishwa cheo kuwa kamanda.

Thumb
Stempu ya posta ya Umoja wa Kisovyeti ya mwaka 1981 iliyotolewa kwa kumbukumbu ya miaka 300 kuzaliwa kwa Bering
Remove ads

Msafara wa kwanza wa Kamchatka

Mnamo mwaka wa 1639 wawindaji Warusi walivuka Bahari Pasifiki kutoka Siberia hadi Amerika ya Kaskazini . [3] Tsar Peter I wa Urusi aliposikia kuhusu safari hiyo alitaka kuwa na uhakika kuhusu ukweli wake. Mnamo 1724 alituma msafara wa kwanza kwenda Kamchatka (1725-30) ulioongozwa na Bering. Shabaha moja ilikuwa kuona kama Siberia imeunganika na Amerika Kaskazini. Walisafiri kwanza hadi Rasi ya Kamchatka ambapo walijenga meli kwa ajili ya upelelezi. Mnamo 1728 Bering alisafiri kaskazini kwa kutosha ili kugundua kuwa Siberia na Amerika Kaskazini (Alaska) haziunganiki. [1] Hapo aliona sehemu ya bahari inayotenganisha Asia na Amerika iliyopokea baadaye jina la Mlangobahari wa Bering kwa heshima yake.

Remove ads

Msafara wa pili wa Kamchatka

Msafara wa pili wa Kamchatka (1733-43) ilikuwa safari kubwa sana ya kisayansi. Iliongozwa pia na Bering. Msafara huo, ulipokuwa njiani, ulituma makundi madogo ya wapelelezi kwenda pande mbalimbali waliochora kwa mara ya kwanza ramani za pwani za Siberia na Bahari Pasifiki. Bering alituma pia meli hadi Japani na Amerika.[1] Bering mwenyewe alifikia Alaska mnamo 1741. Katika safari ya kurudi ilibidi wasimame kwenye kisiwa kilichopokea baadaye jina la Kisiwa cha Bering. Walipokaa kisiwani karibu nusu ya mabaharia wote walifariki, pamoja na Bering.

Mnamo 1991, wataalamu wa akiolojia kutoka Denmark walikuta kaburi lake.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads