Wadruzi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wadruzi (kwa Kiarabu: درزي, derzī au durzī, wingi دروز, durūz; kwa Kiebrania דרוזי, drūzī, wingi דרוזים, druzim) ni watu wenye asili ya Mashariki ya Kati wanaofuata dini yao maalumu inayohusiana na Uislamu[1], Uyahudi na Ukristo lakini inategemea zaidi falsafa, ikiheshimu Plato, Aristotle, Sokrates na Akhenaten.[2][3]




Remove ads
Asili
Al-Hakim, mtawala wa Misri katika karne ya 11 BK, aliunga mkono dini hiyo ambayo ilianzishwa na Hamza bin Ali lakini inamheshimu kuhani Yetro, babamkwe wa Musa, kama nabii mkuu na mwanzilishi wao.
Nyaraka za Hekima ndiyo maandishi ya msingi wa dini hiyo.[4].
Uenezi
Idadi yao si chini ya 1,000,000, ambao nusu yao wanaishi katika mkoa wa Hauran nchini Syria. Waliobaki wanaishi hasa Lebanoni, Israeli, lakini pia Venezuela, Marekani n.k.[5]
Athari katika siasa
Pamoja na uchache wao kati ya dini za Mashariki ya Kati, walikuwa na athari kubwa katika siasa, hasa nchini Lebanoni walipotawala hadi miaka ya 1860, walipogawana madaraka na Wamaroni. Baada ya uhuru wa nchi hiyo walihesabiwa kuwa madhehebu ya 4 kwa ukubwa. Mwanzoni mwa miaka ya 1980 hadi mwishoni mwa 1990 walishika nafasi kubwa katika vita vya kupunguza haki za Wakristo nchini ili kushika nafasi zaidi serikalini.
Tanbihi
Marejeo
Marejeo mengine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads