Wakartusi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Shirika la Wakartusi, au Shirika la Mt. Bruno, ni utawa mmojawapo wa Kanisa Katoliki. Wamonaki wake wote, wanaume kwa wanawake wanaishi ndani kwa ndani: wengine katika nyumba za binafsi, wengine katika makao ya pamoja.




Shirika lilianzishwa na Bruno Mkartusi mwaka 1084.
Linafuata sheria zake, badala ya kanuni ya Benedikto wa Nursia inayoongoza wamonaki karibu wote wa Kanisa la Kilatini.
Jina linatokana na milima ya Chartreuse (nchini Ufaransa), ambapo Bruno na wakaapweke wenzake 6 walijenga makao ya kwanza.
Kaulimbiu ya shirika ni: Stat crux dum volvitur orbis (kwa Kilatini "Msalaba unadumu wakati ulimwengu unabadilikabadilika."
Remove ads
Hatua upwekeni
- Utakaji (miezi 3 hadi 12).
- Unovisi (miaka 2).
- Nadhiri za muda (miaka 3).
- Nadhiri za daima.
Nyumba za Wakartusi leo
Leo duniani ziko nyumba 25 za Wakartusi; kati yake 5 ni za masista. Kwa jumla wako wamonaki 370 wanaume na 75 wanawake. Monasteri hizo ziko Argentina (1), Brazil (1), France (6), Germany (1), Italy (4), Ureno (1), Slovenia (1), South Korea (2), Spain (5), Uswisi (1), Ufalme wa Muungano (1) na Marekani (1).[1]
Filamu
- "Into Great Silence"—the award winning documentary on the hermit monks of the Roman Catholic Carthusian Order
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
