Wasuni

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wasuni
Remove ads

Wasuni ni dhehebu kubwa ndani ya dini ya Uislamu. Takriban asilimia 80 - 90 za Waislamu wote duniani hukadiriwa kuwa Wasuni na wengine 10-20 % huhesabiwa kati ya Washia.

Thumb
Nchi za Waislamu wengi na madhehebu
Kibichi: Wasuni wengi; Nyekundu: Washia wengi

Wasuni huitwa kwa Kiarabu ahl ul-sunna (Kiarabu: أهل السنة; "watu wa mapokeo"). Neno Suni hutokana na neno sunna (kwa Kiarabu : سنة ) inayomaanisha mapokeo ya Mtume Muhammad.

Isipokuwa Uajemi, Iraki, Bahrain, Azerbaijan, Yemen, Omani na Lebanoni kundi hilo ni kubwa katika nchi zote penye Waislamu wengi.

Remove ads

Historia

Wasuni hufuata mwelekeo wa Uislamu ulioanzishwa na ukhalifa wa Abu Bakr na kutokubali uongozi wa familia ya Mtume Muhammad kupitia Ali, Hassan na Husain.

Madhehebu ya Wasuni

Kati ya Wasuni kuna madhehebu nne zinazotofautiana kiasi kuhusu mafundisho ya sharia au sheria ya kidini ya Kiislamu. Ndio Wahanafi, Wamaliki, Washafii na Wahanbali. Kwa jumla Wasuni hukubaliana ya kwamba madhehebu haya yote manne ni sawa.

Walimu wengine hasa katika kikundi cha Wawahabi kilichoanzishwa kati ya Wahanbali kimekaza mafundisho yake hadi kuwashtaki wengine kuwa si Waislamu wa kweli.

Remove ads

Viungo vya Nje

Ukweli wa haraka
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads