Wilaya ya Tarime

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wilaya ya Tarime
Remove ads

Wilaya ya Tarime ni wilaya mojawapo kati ya 9 za Mkoa wa Mara. Zamani ilijulikana kwa jina la "Wilaya ya Mara Kaskazini". Mwaka 2006 sehemu ya mashariki ya Tarime imekuwa wilaya mpya ya Rorya.

Thumb
Mahali pa Tarime (kijani cheusi) katika Mkoa wa Mara (kijani) na Tanzania kwa jumla.
Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...

Tarime imepakana na Kenya (kaunti za Migori, Trans Mara na Kisii) upande wa kaskazini na mashariki. Hifadhi ya wanyama ya Masai Mara ya Kenya uko upande wa mashariki pia. Upande wa kusini umepakana na wilaya za Musoma mjini, Musoma vijijini na wilaya ya Serengeti. Upande wa magharibi iko wilaya mpya ya Rorya.

Makao makuu ya wilaya yapo mjini Tarime.

Misimbo ya posta katika wilaya hii inaanza kwa 314.

Remove ads

Wakazi

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 339,693[1] na katika ile ya mwaka 2022, baada ya kumegwa, walihesabiwa 404,848 [2].

Tarime ni eneo la Wakuria hasa, waliopo pia ng'ambo ya mpaka nchini Kenya. Wakazi asilia wengine ni Wasimbiti.

Wakazi wengi ni wakulima na wafugaji wa wanyama kama vile ng'ombe, mbuzi na kondoo. Eneo la Tarime linajulikana kwa matatizo ya mapigano ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji.

Remove ads

Migodi ya dhahabu

Karibu na kijiji cha Nyamongo katika kata ya Nyamwaga kuna migodi ya dhahabu ya North Mara Gold Mine inayomilikiwa na kampuni Acacia Mining kutoka Uingereza. Kuwepo kandokando kwa utajiri wa dhahabu na umaskini wa wenyeji kunasababisha mara kwa mara kuingia kwa wanavijiji katika eneo la migodi wanapojaribu kukusanya mtapo wenye dhahabu.

Mwaka 2011 na 2013 wanavijiji kadhaa walioingia katika eneo la migodi waliuawa na maafisa wa polisi waliosaidia walinzi wa kampuni[3][4]. Mashirika ya haki za binadamu yalishtaki kampuni kwa niaba ya wahanga mbele ya mahakama huko Uingereza. Kesi zilisimamishwa mwezi wa Fevruari 2015 baada ya kampuni kulipa fidia kwa familia husika.[5][6]

Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads