Mfumo wa Msimbo wa Posta Tanzania

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mfumo wa Msimbo wa Posta Tanzania
Remove ads

Mfumo wa Misimbo ya Posta ya Tanzania (postikodi Tanzania) umeanzishwa tangu mwaka 2012. Msimbo wa posta ni namba iliyochaguliwa kwa kila kata nchini. Kila kata ina msimbo wa tarakimu tano.

Thumb
Mfano wa matumizi ya Msimbo wa Posta katika anwani ya barua (alama nyekundu)

Nia ni kuwa kila barua inayotumwa nchini Tanzania ionyeshe namba hiyo juu ya bahasha yake kama sehemu ya anwani ya barua au kifurushi ili kurahisisha na kuharakisha usafirishaji.

Namba ya msimbo wa posta ni tofauti na namba ya sanduku la posta; msimbo wa posta unahusu mahali au eneo, ilhali sanduku la posta linamhusu mpokeaji wa barua.

Remove ads

Muundo wa tarakimu katika msimbo wa posta wa Tanzania

Msimbo wa posta nchini Tanzania huwa na tarakimu tano zilizopangwa kufuatana na ngazi za utawala wa nchi:

  • tarakimu ya kwanza inaonyesha kanda
  • tarakimu ya pili (pamoja na inayotangulia) inaonyesha mkoa
  • tarakimu ya tatu (pamoja na zinazotangulia) inaonyesha wilaya au halmashauri
  • tarakimu za nne na tano (pamoja na zinazotangulia) zinaonyesha kata.
    • Badala ya kata tarakimu kamili zinaweza kuteuliwa pia kwa ajili ya mteja mkubwa anayepokea barua nyingi sana, au eneo maarufu au shughuli maalumu. Mfano ni kampuni kubwa au wizara kuwa na msimbo wa pekee.
    • Hakuna misimbo ya pekee kwa kata zote za Tanzania; wakati mwingine kata kadhaa za wilaya ileile zimeunganishwa kwa kazi ya posta na kuwa na msimbo mmoja[1]

Mfano:

6 5 4 0 1 ni msimbo wa posta kwa Kilwa Masoko.
6 ni tarakimu kwa Kanda ya Pwani
6 5 inaonyesha Mkoa wa Lindi
6 5 4 inataja Wilaya ya Kilwa (651 ni Lindi mjini, 563 Nachingwea, 655 Liwale, na kadhalika)
• Tarakimu za mwisho 0 1 ni za kata ya Kilwa Masoko.

Ilhali wilaya ya Kilwa huwa na kata 21, misimbo ya kata za Kilwa inaendelea kuanzia 6 5 4 0 1 (Kilwa Masoko) hadi 6 5 4 2 1 (Kibata).

Maana yake kama barua inaonyesha anwani ya „65421 Kibata“ inaweza kusafirishwa, si lazima mfanyakazi aulize Kibata iko wapi? Inatosha akijua ni barua kwenda pwani („6“) na Mkoa wa Lindi („65“). Pale Lindi wanajua wilaya zao na 654 ni Kilwa, vivyo hivyo hao wanajua kata katika eneo lao.

Utaratibu huo unatunza nafasi kwa kuanzishwa kwa vitengo vipya; kanda linaweza kuongezwa mikoa hadi 10, kila mkoa wilaya hadi 10, na kata hadi 100 kila wilaya. Kuna pia nafasi kwa kanda mpya 2.

Remove ads

Kanda

Kanda ni hizi zifuatazo, na kila mkoa wa Tanzania ni sehemu ya kanda fulani:

  1. Dar es Salaam (Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo, Kigamboni)
  2. Kaskazini
  3. Ziwa
  4. Kati
  5. Nyanda za Juu Kusini
  6. Pwani
  7. Zanzibar

Ugawaji wa misimbo ya posta kwenye mikoa na wilaya

1. Kanda ya Dar es Salaam

Maelezo zaidi Eneo, Tarakimu ...

2. Kanda ya Kazkazini

3. Kanda ya Ziwa

Maelezo zaidi Eneo, Tarakimu ...

4. Kanda ya Kati

Maelezo zaidi Eneo, Tarakimu ...

5. Kanda ya Nyanda za Juu Kusini

Maelezo zaidi Eneo, Tarakimu ...

6. Kanda ya Pwani

7. Kanda ya Zanzibar

Maelezo zaidi Eneo, Tarakimu ...
Remove ads

Tanbihi

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads