Wilibaldi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wilibaldi (Wessex, Uingereza, 22 Septemba 700 – Eichstaett, Ujerumani, 7 Julai 787 au 788) alikuwa mmonaki Mbenedikto ambaye, baada ya kuhiji sehemu mbalimbali hadi Nchi takatifu na kustawisha umonaki, alipata umaarufu kwa umisionari wake katika Ujerumani ya leo alipotumwa na Papa Gregori III kumsaidia Bonifasi.

Ndugu zake Winibaldi na Walburga pia walishiriki kazi hiyo.
Alikuwa askofu wa kwanza wa Eichstaett, alipoongoa wengi, akafariki huko[1].
Anaheshimiwa tangu zamani kama mtakatifu, hasa baada ya kutangazwa na Papa Leo VII (938).
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Vyanzo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads