Yezebeli

From Wikipedia, the free encyclopedia

Yezebeli
Remove ads

Yezebeli (kwa Kiebrania אִיזֶבֶל|אִיזָבֶל |Izével|Izável|ʾÎzéḇel|ʾÎzāḇel) alikuwa malkia wa Israeli kama mke wa Mfalme Ahabu katika karne ya 9 KK.

Thumb
Kifo cha Yezebeli kilivyochorwa na Gustave Doré.

Binti wa mfalme Ethbaal wa Tiro, Finisia, alimhimiza mumewe kuachana na imani ya taifa lake katika Mungu pekee, YHWH akaangamiza manabii wake (1Fal 16:21-31 ).

Aliyeokoa imani hiyo ni nabii Elia ambaye katika mlima Karmeli alishinda manabii wa miungu Baal na Ashera waliotunzwa na Yezebeli (1Fal 18).

Kazi yake ilikamilishwa na mwanafunzi wake, nabii Elisha aliyempaka mafuta Yehu awe mfalme na arudishe Israeli kwa Mungu wake. Katika mapinduzi yake, Yezebeli aliuawa kikatili (2Fal 9:1-36) kama alivyotabiri Elia.

Kwa uovu wake, Yezebeli anatajwa na Kitabu cha Ufunuo pia (2:20-23).

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads