Yterbi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Yterbi (Ytterbium) ni elementi ya kimetali yenye alama Yb na namba atomia 70, maana yake kiini cha Yterbi kina protoni 70 ndani yake. Uzani atomia ni 173.045. Katika jedwali la elementi inahesabiwa kati ya lanthanidi na metali za ardhi adimu.

Kiasili Yterbi haipatikani kwa hali safi lakini imo ndani ya madini mengi.
Iligunduliwa mnamo mwaka 1878 wakati mwanakemia Mswisi Jean Charles Galissard de Marignac alitenga kutoka ardhi adimu ya "erbia" na kuiita Ytterbia kutokana na kijiji cha Ytterby, Uswidi ambako aliwahi kupata madini aliyochungulia.[1] [2]
Yterbi ni vigumu kutengwa na madini mengine, kwa hiyo haina matumizi mengi isipokuwa viwango vidogo katika leza kadhaa.
Remove ads
Marejeo
Kusoma zaidi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads