Ytterby
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ytterby ni kijiji kwenye kisiwa cha Resarö, katika Manispaa ya Vaxholm kwenye funguvisiwa la Stockholm nchini Uswidi.

Jina la kijiji linamaanisha "kijiji cha nje". [1] Ytterby ni maarufu kwa sababu katika migodi yake elementi nane zilitambuliwa mara ya kwanza. Elementi nne za Ytri (Y), Yterbi (Yb), Erbi (Er) na Terbi (Tb) zote zimepewa jina la Ytterby.
Remove ads
Ugunduzi wa elementi
Tangu miaka ya 1500 hivi felspar ilichimbwa hapa kwa ajili ya kiwanda cha kauri. Mnamo 1787 luteni Carl Axel Arrhenius aliyechungulia eneo kwa kupata mahali pa kujenga ngome alikuta jiwe jeusi na zito ambalo halikujalikana. [2] Mwaka 1794 jiwe hilo lilifanyiwa utafiti na mtaalamu Johan Gadolin aliyetambua kwamba sehemu kubwa ilikuwa elementi mpya. Mwanakemia wa Uswidi Anders Gustaf Ekeberg alithibitisha ugunduzi huo mwaka uliofuata na akaiita kwa jina la Yttria, na yale madini aliitwa Gadoliniti. [3]
Ndani ya madini ya gadoliniti jumla ya elementi saba ilipatikana.
Mbali na Ytri (Y), Yterbi (Yb), Erbi (Er) na Terbi (Tb), elementi za Scandi (Skandinavia), Holmi (Ho, jina la Stockholm), Thuli (Tm, jina la Thule, kisiwa cha kaskazini katika mitholojia ya Kigiriki) ya Scandinavia), na Gadolini (Gd, jina la mvumbuzi Johan Gadolin) zilitambuliwa katika madini ya Ytterbi. [4]
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads