Yohakimu wa Fiore
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Yohakimu wa Fiore, O.Cist., au wa Flora (kwa Kiitalia Gioacchino da Fiore; Celico, leo mkoani Calabria, 1135 hivi – San Martino di Canale, Calabria, 30 Machi 1202) alikuwa mmonaki wa Italia kusini aliyeanzisha abasia ya San Giovanni in Fiore na shirika la San Giovanni in Fiore lilitokana na lile la Citeaux.[1]

Ni maarufu kwa mafundisho yake ambayo baadaye yalikuja kulaaniwa na Kanisa Katoliki kama ya kizushi.
Hata hivyo mwenyewe hakuwa na nia hiyo, bali alimwekea Papa maamuzi yoyote juu yake. [2]
Kwa sababu hiyo shirika lake, likizingatia uadilifu wake wa kishujaa, liliwahi kumtangaza mwenye heri, na sasa jimbo lake la Cosenza-Bisignano linaendelea na kesi ya kumtambua hata mtakatifu.
Remove ads
Maandishi yake

- Liber Concordiae Novi ac Veteris Testamenti (Harmony of the Old and New Testaments/Book of Concordance), iliyokamilika mwaka 1200.[3]
- Expositio in Apocalipsim (Exposition of the Book of Revelation), iliyokamilika miaka 1196-9. [4]
- Psalterium Decem Cordarum (Psaltery of Ten Strings).[5]
- Tractatus super quatuor Evangelia (Treatise on the four Gospels).[6]
Maandishi mengine ni kama vile:
- Genealogia (Genealogy), iliyoandikwa mwaka 1176.[7]
- De prophetia ignota, iliyoandikwa mwaka 1184.[8]
- Adversus Judeos (also known as Exhortatorium Iudeorum), iliyokamilika mwaka 1180s.[9]
- De articulis fidei, iliyoandikwa miaka ya 1180.[10]
- Professio fidei, iliyoandikwa miaka ya 1180.[11]
- Tractatus in expositionem vite et regule beati Benedicti, hotuba za miaka ya 1180.[12]
- Praephatio super Apocalipsim. iliyoandikwa miaka ya 1188-1192.[13]
- Intelligentia super calathis. iliyoandikwa miaka ya 1190-1.[14]
- De ultimis tribulationibus, hotuba fupi.[15]
- Enchiridion super Apocalypsim. iliyoandikwa miaka ya 1194-6, toleo la awali la Liber introductorius iliyo dibaji ya Expositio in Apocalipsim.[16]
- De septem sigillis.[17]
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads