Yohane Mbatizaji wa Rossi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Yohane Mbatizaji wa Rossi
Remove ads

Yohane Mbatizaji wa Rossi (kwa Kiitalia: Giovanni Battista de' Rossi; Voltaggio, Piemonte, 22 Februari 1698Roma, Lazio, 23 Mei 1764) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Italia.

Thumb
Mt. Yohane Mbatizaji wa Rossi.

Papa Pius IX alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Mei 1860, halafu Papa Leo XIII akamtangaza mtakatifu tarehe 8 Desemba 1881[1].

Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake[2].

Remove ads

Maisha

Mtoto wa maskini, alikwenda Roma kwa masomo[3] akapewa upadrisho ingawa alikuwa ameanza kuugua kifafa kilichomsumbua hadi mwisho wa maisha yake.

Tangu hapo alijitosa kuhudumia fukara na waliotengwa na jamii, wakiwa pamoja na wanawake, wagonjwa, wafungwa, wafanyakazi, akiwapa pia mafundisho ya Kikristo mbali ya kuadhimisha sakramenti ya upatanisho kwa wengi[4].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads