Kalenda ya Kiyahudi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kalenda ya Kiyahudi (pia: Kalenda ya Kiebrania) ni kalenda inayotumiwa katika dini ya Uyahudi na pia nchini Israeli. Inatumiwa kupanga tarehe za sikukuu za Kiyahudi na utaratibu wa kusoma Torati kwa kila wiki.
Mwaka
Kalenda hiyo inajua miaka tofauti ndani ya kipindi kilekile.
Kanuni za msingi
Kalenda ya Kiebrania ni kalenda jua-mwezi.
- Miezi ya kalenda hiyo hufuata mwonekano halisi wa Mwezi angani, sawa na kalenda ya Kiislamu. Mwezi mpya unaanza wakati wa kuonekana kwa hilali.
- Wakati huo huo, Pasaka ya Kiyahudi inapaswa kutokea kwenye majira ya machipuo, wakati wa mwezi Aprili au mwisho wa Machi. Ilhali majira ya machipuo hufuata mwendo wa Jua, kanuni hii inafunga makadirio ya mwaka na mwendo wa Jua.
- Hii inasababisha ulazima wa kupatanisha tofauti kati ya muda wa mwaka wa Jua (siku 365) na muda wa mwaka wa Mwezi (takriban siku 354).
- Hapo kalenda ya Kiebrania inaongeza mwezi wa nyongeza mara saba katika kila kipindi cha miaka 19. Kwa hiyo kuna miaka ya kawaida yenye siku 354 na miezi 12. Lakini kila mwaka wa pili au wa tatu ni mwaka mrefu wenye miezi 13 na siku 384.
Remove ads
Juma
Nje ya kalenda hiyo kuna utaratibu wa wiki ya siku saba zinazoendelea mfululizo, sawa na kalenda ya kimataifa. Hutumiwa kubaini siku ya Shabbat, ambayo ni siku ya kupumzika. Wiki haitegemei mwaka wa jua wala wa mwezi. Badala yake, inategemea hesabu ya siku saba ambazo zinaaminika kurudi nyakati za zamani za Babeli na kutajwa katika masimulizi ya kuumbwa kwa Dunia katika Biblia.
Siku za juma la Kiyahudi
Remove ads
Miezi
Siku na wiki
Katika kalenda ya Kiyahudi, siku inafafanuliwa kufuatana na Biblia ya Kiebrania: [2] "Na ilikuwa jioni, na ilikuwa asubuhi, siku moja". Kwa sababu "jioni" inakuja kabla ya "asubuhi", siku katika kalenda ya Kiyahudi huanza jioni baada ya machweo . Ni muhimu kuhakikisha kuwa siku iliyopita imekwisha kabisa, hivyo siku mpya huanza wakati wa usiku umeanza. [3]
Katika kalenda zinazochapishwa, tofauti hii haionekani maana hapa tarehe za kalenda ya Kiyahudi na tarehe za Kalenda ya Gregori zinazoanza usiku wa manane huonyeshwa kandokando. Ineleweka kuwa watu wanaotumia kalenda hizi wanajua utaratibu wa kuanza siku baada ya machweo. Wakati wowote sikukuu, siku ya kuzaliwa au ya kumbukumbu ikionekana kwenye kalenda iliyochapishwa, kwa kweli huanza jioni iliyotangulia, baada ya machweo.
Molad
Hesabu ya kalenda ya Kiebrania mwaka na mwezi huanza na molad inayomaanisha hilali. Molad ni neno la Kiebrania linalomaanisha "kuzaliwa". Neno hilo linamaanisha "kuzaliwa" kwa mwezi mpya kila mwezi. Kalenda ya kisasa ya Kiebrania hutumia molad iliyohesabiwa: urefu wa wastani wa muda kutoka mwezi mpya hadi mwezi mpya. Urefu wa Molad ni siku 29, masaa 12, dakika 44, sekunde 3 na nusu. [4]
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Tovuti nyingine
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads