Sukkot

From Wikipedia, the free encyclopedia

Sukkot
Remove ads

Sukkot (pia inajulikana kama Sikukuu ya Vibanda) ni sikukuu ya Kiyahudi. Katika tukio hilo, watu husherehekea ukusanyaji wa mazao ya matunda[1], na kukumbuka wakati uliopita Wayahudi walipokaa katika vibanda vidogo walipokuwa kwenye safari ya kutoka Misri kuelekea Kanaani[2].

Thumb
Kibanda cha Sukkot nchini Israeli
Thumb
Sukkot kati ya nyumba

Asili

Sukkot ni kati ya sikukuu zinazoamriwa katika Torati [3].

Sherehe hizo za mavuno zimeunganishwa na kumbukumbu ya historia ya Israeli. Wayahudi wanakumbuka uhamiaji wa miaka arobaini kutoka Misri kupitia jangwa la Sinai hadi "Nchi ya Ahadi" ya Kanaani. Wakati huo waliishi katika vibanda ambavyo walivijenga tena na tena kwa matawi makavu ya mitende. Kwa ukumbusho wa jambo hilo wanakaa katika vibanda vya kujitengenezea kwa muda wa siku saba kila mwaka.

Remove ads

Desturi

Vibanda vya Sukkot ya leo hutengenezwa kwa mbao, matawi, majani na nguo na kupambwa kwa maua na matunda. Paa hujengwa kwa matawi na majani na inasemekana kuwa kiasi cha kutosha kutoa kivuli kwenye jua la mchana na kuwa na nafasi kiasi cha kuona nyota usiku. Kibanda kicho huwekwa kwenye bustani kama iko au pia kwenye roshani. Katika masinagogi mengi, maskani hujengwa katika ua wa sinagogi, ambayo inaweza kutumika kwa uhuru na wanajamii.

Mbali na kibanda, shada maalum ni muhimu kwa sherehe ya Sukkot: imefungwa pamoja kwa matawi ya mitende na vichaka vingine. Shada hilo hushikwa kwenye sinagogi kwa mkono mmoja huku mkono mwingine hushika aina ya limau kama ishara ya tunda la paradiso ambalo lina harufu nzuri sana.

Remove ads

Tarehe

Sukkot husheherekewa kwa siku saba (lakini nje ya nchi ya Israeli kwa siku moja pekee) kwenye tarehe 15 hadi 21 mwezi wa Tishri. Tarehe kwenye kalenda ya Gregori zinafuata. Sherehe inaanza jioni ya siku inayotangulia tarehe ya kwanza inayotajwa: [4]

  • 2021: 21-27 Septemba
  • 2022: 10-16 Oktoba
  • 2023: 30 Septemba - 6 Oktoba
  • 2024: 17-23 Oktoba
  • 2025: 7-13 Oktoba

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads