From Wikipedia, the free encyclopedia
Kitabu cha Sefania ni kimojawapo kati ya vitabu vya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), hivyo kinapatikana pia katika Agano la Kale ambalo ni sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.
Kutokana na ufupi wake kimepangwa tangu kale kati ya vitabu 12 vya Manabii Wadogo.
Nabii Sefania, mtu wa Yerusalemu alihubiri kwa nguvu (640-625 hivi K.K.) mwanzoni mwa utawala wa mfalme Yosia, kabla huyo hajaanza urekebisho wake wa kidini uliofuata kuvumbua katika hekaluni maandiko ya Kumbukumbu la Sheria.
Pamoja na kutisha kwa matabiri yake, aliahidi wokovu kwa mabaki ya Israeli, akisema watakuwa watu maskini na walioonewa (3:9-20).
Ndio mwanzo wa imani ya kuwa wapenzi wa Mungu ni hasa mafukara, atakavyosisitiza Yesu (Lk 6:20-21).
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.