Moravia (kwa Kicheki na Kislovakia: Morava; kwa Kijerumani: Mähren; kwa Kihungaria: Morvaország; kwa Kipoland: Morawy) ni mkoa wa kihistoria mashariki mwa Ucheki.

Thumb
Moravia
Thumb
Bendera ya Moravia[1][2]
Thumb
Moravia katika jamhuri ya Ucheki

Jina limetokana na mto Morava. Jina la Moravia linatumiwa na Kanisa la Kiprotestanti linalojulikana katika nchi nyingi kama "Kanisa la Moravian".

Pamoja na Bohemia eneo la Moravia ni sehemu muhimu ya Ucheki, nchi iliyoanzishwa mwaka 1993 baada ya Slovakia kutoka katika Chekoslovakia.

Mji mkuu wa Moravia ni mji wa Brno (Kijer.: Brünn).

Historia

Moravia imekaliwa na makabila ya Waslavoni tangu karne ya 6.

Katika karne ya 9 milki ya Moravia ilikuwa nchi muhimu zaidi kati ya Waslavoni wa Ulaya, lakini mwanzoni mwa karne ya 10 iliporomoka kutokana na ueneaji wa Ujerumani upande wa magharibi na wa Hungaria upande wa mashariki-kusini.

Baadaye watawala wa Bohemia na Moravia walialika Wajerumani kuhamia na kuunda miji na vijiji. Hivyo takriban 1/3 ya wakazi wa Moravia waliongea Kijerumani hadi mwaka 1945 wakati Wajerumani walipofukuzwa katika Chekoslovakia.

Katika karne zilizofuata Moravia ilikuwa chini ya athira ya Poland au Ujerumani ikaendelea kuwa sehemu ya Dola Takatifu la Kiroma na tangu mwaka 1526 chini ya utawala wa familia ya Habsburg na baadaye ilitawaliwa kama sehemu ya milki ya Austria.

Wakati wa kusambaratishwa kwa Austria-Hungaria mwaka 1918 Moravia ilifanywa sehemu ya nchi ya Chekoslovakia na tangu mwaka 1993 ya Ucheki.

Tanbihi

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.