Adama Barrow
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Adama Barrow (*16 Februari 1965) ni rais wa Gambia na mwanasiasa wa chama cha United Democratic Party.[1]

Remove ads
Utoto na shule
Barrow alizaliwa katika kijiji cha Mankamang Kunda karibu na Basse. Alisoma shule ya msingi Koba Kunda na shule ya sekondari Crab Island mjini Banjul. Baadaye alipata nafasi kwenye Muslim High School ya Banjul.
Kazi
Baada ya kufaulu aliajiriwa na kampuni ya Alhagie Musa & Sons na akapandishwa cheo hadi kuwa muuzaji mkuu.[2]
Baada ya mwaka 2000 Barrow alihamia London aliposoma uchumi. Wakati huu alifanya kazi ya usiku kama mlinzi wa nyumba kwa kujipatia riziki. [3]
Baada ya kurudi Gambia mwaka 2006 alianzisha kampuni ya Majum Real Estate akawa meneja mkuu hadi sasa.[2]
Siasa
Mwaka 2016 Barrow alichaguliwa kuwa mgombea wa urais katika mkutano wa vyama 7 vya upinzani. [4][5]
Tarehe 2 Desemba 2016 Barrow alishtusha taifa kwa kumshinda Yammeh katika uchaguzi wa urais [6][7] kwa kupata kura 263,000 au asilimia 45 za kura zote dhidi ya kura 212,000 au asilimia 36 kwa rais Yahya Jammeh. Mgombea wa tatu Mama Kandeh alipata asilimia 17.
Kwanza Rais Yahya Jammeh alikubali kushindwa hata kabla ya tangazo rasmi la matokeo[8][9], lakini siku nane baadaye alianza kung'ang'ania madaraka.
Kufuatana na katiba rais Adama Barrows alitakiwa kuapishwa takribani siku 60 baada ya uchaguzi.[10], lakini tarehe 9 Disemba 2016 rais Jammeh alitangaza ya kwamba hakubali matokeo akitaka uchaguzi mpya.[11]
Tarehe 19 Januari 2017, rais mteule aliapishwa katika ubalozi wa Gambia huko Dakar, halafu wanajeshi wa Senegal, Nigeria na Ghana walivamia nchi ili kumuondoa madarakani kwa idhini ya Umoja wa Mataifa.
Mnamo Novemba 2021, Adama Barrow alitangaza kugombea tena nafasi ya uraisi mwaka 2024.
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads