Banjul

From Wikipedia, the free encyclopedia

Banjul
Remove ads

Banjul ni mji mkuu wa Gambia. Mji wenyewe una wakazi 34,828 pekee[1] lakini pamoja na mitaa ya nje ni zaidi ya nusu milioni.

Ukweli wa haraka Nchi, Mji ...
Thumb
Muonekano wa Mji wa Banjul
Thumb
Mahali pa Banjul katika Gambia
Thumb
Banjul mjini
Thumb
Geti ya Arch 22 ya kuingia mji wa Banjul

Banjul iko kwenye kisiwa cha Mt. Mariamu (au: Kisiwa cha Banjul) mdomoni mwa mto Gambia unapoishia katika bahari ya Atlantiki.

Remove ads

Historia

Waingereza walianzisha mji mwaka 1816 BK kama kituo cha biashara na kituo cha kijeshi cha kukomesha biashara ya watumwa. Jina la mji lilikuwa "Bathurst" kufuatana na Henry Bathurst aliyekuwa waziri wa makoloni wakati ule.

Mwaka 1965 Bathurst ilikuwa mji mkuu wa nchi huru ya Gambia. Mwaka 1973 jina lilibadilishwa kuwa Banjul. Tarehe 22 Julai 1994 palikuwa na mapinduzi wa kijeshi yaliyoanzisha utawala wa Rais Yahaya Jammeh. Geti la mji "Arch 22" lilijengwa kama kumbukumbu ya mapinduzi haya.

Remove ads

Uchumi

Banjul ni kitovu cha utawala na biashara katika Gambia.

Mawasiliano ndani ya nchi ni hasa kwa njia ya feri kwenye mto Gambia hadi mji wa Barra.

Msingi wa uchumi ni kilimo, hasa karanga, nta, mawese na ngozi zinasafirishwa kutoka bandari ya Banjul.

Banjul ina uwanja wa ndege wa kimataifa.

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads