Kiwolofu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kiwolofu ni lugha iongewayo nchini Senegal, Gambia, na Mauritania. Lahaja za Kiwolofu zinaweza kufanana sana kati ya nchi hizo, zikiwa sambamba kabisa kitabia na hata kuongelewa kieneo.

Lugha hiyo ipo kama lugha jirani ya Kifula inayohesabiwa kati ya lugha za Kisenegambia[1] ya familia ya Lugha za Kiniger-Kongo.
Ni lugha hasa ya Wawolofu, lakini nchini Senegal haizungumzwi na Wawolofu tu, bali hata Wasenegal wengine huzumgumza lugha hiyo; hivyo karibuni asilimia 40 ya wakazi wake huizungumza kama lugha mama.
Idadi ya wasemaji kama lugha mama ni takriban milioni 3.2 na karibu idadi ileile hutumia Kiwolofu kama lugha ya pili.
Kuna lahaja mbalimbali kama vile "Dakar-Wolof". Dakar ni mji wenye watu mchanganyiko, yaani kuna waongeaji wa Kiwolofu, Kifaransa, Kiarabu, na hata Kiingereza huzungumzwa kidogo katika mji huo ambao uko nchini Senegal; hivyo Kiwolofu chao ni cha mchanganyiko.
Maeneo mengine ya Kiwolofu ni kama vile:
- Loukala
- Saint Louis
- Casamanca
- Banjul
- Nouakchott
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads