Gambia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Gambia, kirasmi Jamhuri ya Gambia, ni nchi ndogo kabisa ya Afrika bara. Eneo lake lote linazungukwa na Senegal kwa kufuata mwendo wa mto Gambia hadi Bahari ya Atlantiki.
Kimsingi nchi yote ni maeneo ya kandokando ya mto huo; urefu ni takriban km 500, upana kati ya 10 na 50.
Remove ads
Historia
Zamani eneo la Gambia lilikuwa sehemu ya Dola la Mali na Dola la Songhai.
Nchi kama ilivyo leo imepatikana kutokana na mvutano kati ya Uingereza na Ufaransa wakati wa ukoloni.
Mwanzoni Uingereza ulitafuta tu njia ya maji kwa ajili ya biashara, bila kujali utawala wa nchi.
Mapatano kati ya Ufaransa na Uingereza baada ya vita vya Napoleon Bonaparte yaliimarisha hali hiyo. Wafaransa walichukua eneo lote kubwa la Senegal, na Waingereza ile kanda ndogo ndani ya Senegal.
Tangu uhuru wa nchi zote mbili palikuwa na mpango wa kuziunganisha kwa njia ya shirikisho lililoanzishwa mwaka 1982 lakini Gambia ilitoka katika mapatano hayo mwaka 1989.
Hadi mwaka 1994 Gambia ilifuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi lakini mwaka ule uasi wa wanajeshi ulipindua serikali na kuwa chanzo cha utawala wa Yahya Jammeh aliyekuwa kiongozi, kwanza kama mwenyekiti wa kamati ya kijeshi, baadaye kama rais aliyechaguliwa mwaka 1996 na kuchaguliwa tena miaka 2001, 2006 na 2011. Isipokuwa mwaka 2001 wapinzani na watazamaji wa nje walilalamika ya kwamba kura hazikuwa huru.
Mwaka 2013 Jammeh alitoa Gambia katika Jumuiya ya Madola kama chombo cha ukoloni mamboleo.
Mwaka 2015 Jammeh alitangaza Gambia kuwa nchi ya Kiislamu.
Katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2016 vyama vya upinzani viliungana, na mgombea wao Adama Barrow alishinda, ilhali Jammeh awali alikubali kushindwa, lakini baada ya siku nane alitangaza ya kwamba alitaka kubatilisha matokeo na kuwa na uchaguzi mpya.[3]
Wananchi walianza kukimbilia nchini Senegal.
Tarehe 19 Januari 2017, rais mteule aliapishwa katika ubalozi wa Gambia huko Dakar, halafu wanajeshi wa Senegal, Nigeria na Ghana walivamia nchi ili kumuondoa madarakani kwa idhini ya Umoja wa Mataifa.
Tarehe 21 Januari Jammeh alikubali kuachia. Mwandamizi wake amerudisha nchi katika Jumuiya ya Madola.
Remove ads
Wakazi
Wakazi wa nchi ni hasa wa kabila la Wamandinka, halafu Wafulani na Wawolof, jumla milioni 1.9 hivi.
Lugha rasmi ni Kiarabu, si tena Kiingereza (kuanzia mwaka 2016).
Upande wa dini, Uislamu unafuatwa na 90% za wakazi, Ukristo (hasa Kanisa Katoliki) na 8%, wakati wafuasi wa dini asilia za Kiafrika ni 2%.
Uchumi
Uchumi unategemea kilimo, uvuvi na hasa utalii. Mwaka 2008, thuluthi moja ya wananchi hawakuwa na kipato cha $ 1.25 kwa siku.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads