Adomnani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Adomnani (pia: Adomnán, Adamnán, Adamnanus, Adhamhnán, Eunan; Ireland Kaskazini, 624 hivi - Iona, Uskoti, 704 hivi) mmonaki padri aliyeongoza kama abati monasteri ya kisiwa cha Iona huko Uskoti tangu mwaka 679 hivi hadi kifo chake[1].

Mwenye ujuzi mkubwa wa Biblia ya Kikristo na mpenzi wa umoja na amani asiyechoka kuvipigania, kwa mahubiri yake alisaidia wengi katika Ireland na Uskoti vilevile kukubali maamuzi ya Sinodi ya Whitby kuhusu kuadhimisha sherehe ya Pasaka kwa kufuata mapokeo ya Kanisa la Roma badala ya yale ya Ukristo wa Kiselti[2].
Yeye aliandika maisha ya Kolumba[3], jamaa wa baba yake[4], na Beda Mheshimiwa aliandika juu ya Adomnani mwenyewe aliyemfahamu mapema.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana[5] kama mtakatifu.
Sikukuu yao ni tarehe 23 Septemba[6].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Vyanzo
Marejeo mengine
Marejeo mengine tena
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads