Aldegunda
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Aldegunda (Cousolre, Ufaransa 639 hivi - Maubeuge, Ufaransa, 684 hivi) alikuwa mwanamke aliyeanzisha monasteri pacha na kuziongoza kama abesi chini ya kanuni ya Kolumbani wakati wa mfalme Dagobati II [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu bikira.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Januari[2].
Maisha
Mtoto wa wazazi wa koo mashuhuri, aliongokea Ukristo akabatizwa kwa juhudi za Amando wa Maastricht, akifuatwa na baba yake, ambaye akawa baadaye mtakatifu Walbert. Pia mama yake Bertila na dada yake Vatrude[3][4] ni watakatifu[5].
Baada ya kukataa kuolewa, alitawa[6].
Alivumilia kwa ushujaa maumivu ya saratani ya matiti ambayo ikaja kumuua[7].
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads