Vatrude

From Wikipedia, the free encyclopedia

Vatrude
Remove ads

Vatrude (pia: Waudru; Waldetrudis; Waltraud; Valdetrudis, Valtrudis, Waltrudis; Cousolre, Ufaransa 612 hivi - Mons, leo nchini Ubelgiji, 687 hivi), alikuwa mwanamke aliyeanzisha monasteri na kuiongoza kama abesi chini ya kanuni ya Kolumbani.

Thumb
Sanamu yake.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Aprili[1].

Maisha

Mtoto wa wazazi wa koo mashuhuri, Walbert na Bertila[2], na dada wa Aldegunda, aliolewa na Visenti Madelgari na kumzalia watoto 4 (Landeriki, Dentelini, Aldetruda na Madelberta), ambao wote nane ni watakatifu[3][4].

Watoto walipokuwa wamekua, mumewe alitawa, na miaka miwili baadaye hata yeye alijifungia upwekeni, ila alifuatwa na wanawake wengi[5].

Tanbihi

Tazama pia

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads