Cabo Verde
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Cabo Verde,rasmi Jamhuri ya Cabo Verde (kwa Kireno: República de Cabo Verde), ni nchi ya visiwa iliyoko katika Bahari ya Atlantiki ya Kaskazini, takriban kilomita 570 magharibi mwa pwani ya Afrika ya Magharibi. Inajumuisha visiwa kumi vya asili ya volkeno vilivyogawanywa katika makundi mawili: Visiwa vya Barlavento (kaskazini) na Visiwa vya Sotavento (kusini). Mji mkuu wake ni Praia, ulioko katika kisiwa cha Santiago, ambacho pia ni kisiwa chenye watu wengi zaidi. Cabo Verde ina wakazi takriban 603,901 (2023) na eneo la kilomita za mraba 4,033.
Remove ads
Cabo Verde ni jamhuri ya bunge yenye serikali thabiti ya kidemokrasia, ikiongozwa na Rais José Maria Neves na Waziri Mkuu Ulisses Correia e Silva. Lugha rasmi ni Kireno, ingawa Kikaboverde kinazungumzwa sana katika maisha ya kila siku. Uchumi wa nchi unategemea zaidi sekta ya huduma kama vile utalii, fedha kutoka kwa raia wanaoishi ughaibuni, na uvuvi. Pato la taifa kwa kila mtu lilifikia dola 4,503 kwa mwaka 2023. Licha ya kuwa na rasilimali chache za asili, Cabo Verde imepata mafanikio makubwa katika elimu, afya, na utawala bora, na inaonyesha kiwango cha juu cha maendeleo ya binadamu katika Afrika ya Magharibi.
Remove ads
Jiografia
Eneo la visiwa vyake kwa jumla ni km² 4,033.
Funguvisiwa lake lina visiwa 15 katika vikundi viwili:
- Visiwa "juu ya upepo" (Barlavento): Santo Antão, São Vicente, São Nicolau, Sal, Boa Vista na visiwa bila watu vya Santa Luzia, Branco na Razo.
- Visiwa "chini ya upepo" (Sotavento): Maio, Santiago, Fogo, Brava na visiwa bila watu vya Ilheus Secos ou do Rombo.
Miji
Mji mkuu ni Praia katika kisiwa cha Santiago.
Miji mikubwa zaidi ni (takwimu za mwaka 2010): Praia (wakazi 127,832), Mindelo (wakazi 70,468), Santa Maria (wakazi 23,839), Assomada (wakazi 12,026), Pedra Badejo (wakazi 9,345) na São Filipe (wakazi 8,125).
Historia
Hadi kufika kwa Wareno katika karne ya 15 visiwa vya Cabo Verde havikuwa na watu.
Wareno walianzisha mashamba ya miwa na kuleta watumwa kutoka bara la Afrika.
Cabo Verde ilikuwa pia kituo muhimu cha biashara ya watumwa kati ya Afrika na Amerika.
Wahamiaji kutoka Ulaya walikuwa pia Wahispania, Waitalia pamoja na Wayahudi na Waislamu waliokataliwa kukaa kwao Ureno.
Watu
Kutokana na historia hiyo, leo idadi kubwa ya wakazi ni machotara waliozaliwa na Waafrika (waliochangia 56% ya DNA) na Wazungu (waliochangia 44%).
Lugha rasmi ni Kireno, lakini wakazi wanazungumza zaidi aina mbalimbali za Krioli iliyotokana na lugha hiyo.
Upande wa dini, walau 89.1% ya wakazi ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (78.7%), lakini pia wa madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (10.4%).
Kutokana na hali ngumu ya uchumi, wananchi wanaoishi nje ya Cabo Verde ni mara mbili kuliko wale wanaoishi nchini. Kati ya waliohama baada ya uhuru (1975), 500,000 wanaishi Marekani na 150,000 Ureno. Hata hivyo kuna wahamiaji vilevile, hasa kutoka nchi za Afrika bara.
Remove ads
Tazama pia
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads