Cedd
Askofu wa London; Mtakatifu From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Cedd (pia: Cedda, Ceddus; 620 hivi - 26 Oktoba 664) alikuwa mmonaki katika monasteri wa Lindisfarne huko Uingereza, hadi alipotumwa kuinjilisha Waanglia-Saksoni akafanywa na abati Finano wa Lindisfarne askofu wa London.

Alijitahidi kufanya uchungaji kwa ukamilifu wa maisha kufuatana na mifano bora ya Mababu wa Kanisa.
Pamoja na mdogo wake Chad wa Mercia[1] anasifiwa kwa kuweka misingi ya Ukristo kati ya Wasaksoni wa Mashariki[2] ambao wakati huo walikuwa na ufukara mkubwa.[3].
Alishiriki Sinodi ya Whitby akipatanisha[4] misimamo ya pande mbili zilizopingana[5].
Pia alianzisha monasteri mbalimbali.
Wote wawili wanaheshimiwa tangu kale kama watakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Vyanzo
Marejeo mengine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads