Chapanya

From Wikipedia, the free encyclopedia

Chapanya
Remove ads

Chapanya ni spishi ya nyoka pekee ya jenasi Pseudaspis katika familia Lamprophiidae. Anaitwa jina hili kwa sababu hula panya.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...

Spishi hii ni mrefu kiasi, kwa wastani m 1-1.3 lakini hadi m 1.8. Kichwa ni kidogo chenye pua fupi na bapa. Waliokomaa wana rangi moja tu: machungwa, kahawia, kijivu au nyeusi. Wachanga wana rangi zilizoiva na mabaka meusi au kahawia.

Chapanya huwinda wagugunaji katika vishimo vyao. Kinyume na jina lake hukamata mafuko hasa. Lakini wachanga hula mijusi.

Nyoka huyu hana sumu. Akitishwa anatoa sauti ya kuchata na kududia mwili na kupiga mdomo ukifunguliwa kabisa. Lakini hang'ati sana.

Remove ads

Picha

Marejeo

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chapanya kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads