Denis wa Paris

From Wikipedia, the free encyclopedia

Denis wa Paris
Remove ads

Denis wa Paris alikuwa Mkristo wa karne ya 3 kutoka Roma (Italia).

Thumb
Sanamu ya Mt. Denis akishika fuvu la kichwa chake, Notre Dame de Paris, Ufaransa.
Thumb
Kifodini cha Mt. Denis na wenzake, Basilika la Mt. Denis.

Kadiri ya wanahistoria Wakristo[1]. chini ya kaisari Decius (250 BK), Papa Fabian alituma maaskofu 7 kutoka Roma kwenda Gallia (Ufaransa wa leo) wakahubiri Injili: Grasyano huko Tours, Trofimo huko Arles, Paulo huko Narbonne, Saturnini huko Toulouse, Denis huko Paris, Austremoni huko Clermont na Martial huko Limoges.

Akiwa askofu wa Paris (Ufaransa) aliuawa pamoja na padri Eleuteri na shemasi Rustiko kwa kukatwa kichwa kwa sababu ya imani yake [2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Oktoba[3].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads