Austremoni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Austremoni (alifariki Clermont Ferrand, Akwitania, leo nchini Ufaransa, 286 hivi) alikuwa askofu kutoka Roma ambaye aliinjilisha mji wa Clermont Ferrand na Auvergne kwa jumla[1][2][3].

Kadiri ya wanahistoria Wakristo[4]. chini ya kaisari Decius (250 BK), Papa Fabian alituma maaskofu 7 kutoka Roma kwenda Gallia (Ufaransa wa leo) wakahubiri Injili: Grasyano huko Tours, Trofimo huko Arles, Paulo huko Narbonne, Saturnini huko Toulouse, Denis huko Paris, Austremoni huko Clermont na Martial huko Limoges.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads