Daudi wa Wales
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
David wa Wales (kwa Kiwelisi 'Dewi Sant'; 500 hivi[1] - 589 hivi[2][3]) alikuwa mmonaki wa Welisi, halafu askofu wa Mynyw (sasa inaitwa St Davids kwa heshima yake).
Alitunga kanuni ya kimonaki kwa monasteri aliyoianzisha kwa kufuata mfano na desturi za mababu wa mashariki na alipinga vikali Upelaji. Wafuasi wake wengi waliinjilisha Welisi na nchi za kandokando (Ireland, Cornwall na Bretagne).[4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na msimamizi wa Wales. Mwaka 1120 Papa Kalisti II alithibitisha heshima hiyo[5].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads