Domobeleshi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Domobeleshi
Remove ads

Domobeleshi ni nyoka wasio na sumu wa jenasi Prosymna katika familia Lamprophiidae. Wamepewa jina hili kwa sababu hutumia domo lao kwa kuchimba kama beleshi.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Nyoka hawa ni wafupi, sm 45 kwa kipeo lakini sm 25-35 kwa kawaida. Rangi yao ni kijivu au kahawia mara nyingi pamoja na vidoa vyeusi au kijivubuluu. Spishi nyingine zina mabaka na nyingine zina rangi kali.

Domobeleshi huchimba katika udongo au mchanga mtifu ambapo hutafuta mayai ya mijusi na nyoka wengine. Hawaonekani sana isipokuwa wakati wa mvua.

Nyoka hawa hawana sumu kwa sababu hula mayai ya reptilia wengine tu. Kwa hivyo wanaweza kukamatwa bila shida. Lakini wakitishwa spishi kadhaa hujipinda katika zongomo na wakiguswa huzongoa na kuzonga tena upesi.

Remove ads

Spishi

Remove ads

Marejeo

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Domobeleshi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads