Eleazari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Eleazari (kwa Kiebrania: אֶלְעָזָר, ʼElʽazar au ʼElʽāzār; maana yake "Mungu amesaidia") alikuwa kuhani mkuu wa pili katika Biblia ya Kiebrania baada ya kifo cha baba yake Aroni[1], kaka wa Musa.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Septemba au 30 Julai[2].
Wengine walioitwa Eleazari katika Biblia
Wanaume wengine sita wanatajwa kwa jina hilo katika Biblia:
- Eleazari bin Aminadab, aliyetunza Sanduku la Agano
- Eleazari bin Dodo, shujaa wa Mfalme Daudi
- Eleazari bin Pinhas, aliyetunza vyombo vitakatifu vilivyorudishwa Yerusalemu baada ya Uhamisho wa Babeli
- Eleazari Avaran, aliyeua tembo vitani
- Eleazari mfiadini, aliyeuawa katika dhuluma ya Antioko IV Epifane
- Eleazari bin Eliudi, baba mzaa babu wa Yosefu (mume wa Maria).
Jina hilo liliandikwa kwa Kigiriki "Lazaro", kama kwa rafiki wa Yesu Lazaro wa Bethania.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads