Lazaro wa Bethania

From Wikipedia, the free encyclopedia

Lazaro wa Bethania
Remove ads

Lazaro (kwa Kiebrania אלעזר, Eleazar au Eliezer) ni mtu anayetajwa katika Injili ya Yohane: aliishi katika karne ya 1 huko Bethania, kijiji karibu na Yerusalemu, pamoja na dada zake Martha na Maria.

Thumb
Ufufuko wa Lazaro, Bible Card illustration, 1905.
Thumb
Ufufuko wa Lazaro ulivyochorwa na Juan de Flandes (1500-1510)

Yesu Kristo alifurahia urafiki wao wote, hasa alipokuwa akihiji kwenda Yerusalemu.

Katika nafasi ya mwisho ya kufanya hivyo, alimfufua siku ya nne baada ya kifo chake, jambo lililofanya wengi wamuamini kuwa ndiye Kristo, lakini pia wapinzani wake waharakishe kifo chake mwenyewe[1].

Lazaro anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, na Waorthodoksi na wengineo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa pamoja na ya dada zake[2] tarehe 29 Julai[3].

Remove ads

Michoro ya Ufufuko wa Lazaro

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads