Fungo-bukini

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fungo-bukini
Remove ads

Fungo-bukini ni wanyama wadogo hadi wakubwa kiasi wa Madagaska wanaoainishwa katika nusufamilia Euplerinae wa familia Eupleridae na ambao wanafanana na fungo wa bara la Afrika. Pamoja na nguchiro-bukini (nusufamilia Galidiinae) wana mhenga mmoja aliyekuwa aina ya nguchiro na aliyevuka Mlango wa Msumbiji miaka milioni 20 iliyopita.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Wanyama hawa ni kama fungo wadogo au nguchiro, isipokuwa fosa. Mdogo kuliko wote ni fungo-bukini miraba (sm 20 na g 1500-2000) na mkubwa ni fosa (sm 70-80 na kg 5.5-8.6). Rangi yao ni kahawia au kahawianyekundu.

Wanatokea misituni na hula vertebrata kama lemuri, tandaraka, wagugunaji, mijusi na ndege (fosa na fungo-bukini miraba) au invertebrata kama nyungunyungu, konokono, konokono uchi na lava (falanuki).

Remove ads

Spishi

  • Cryptoprocta ferox, Fosa au Fungo-bukini Mkubwa (Fossa)
  • Eupleres goudotii, Falanuki Mashariki au Fungo-bukini Kahawia Mashariki (Eastern falanouc)
  • Eupleres major, Falanuki Magharibi au Fungo-bukini Kahawia Magharibi (Western Falanouc)
  • Fossa fossana, Fungo-bukini Miraba (Malagasy civet au Fanaloka)

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads