Nguchiro-bukini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nguchiro-bukini ni wanyama wadogo wa Madagaska wanaoainishwa katika nusufamilia Galidiinae wa familia Eupleridae na ambao wanafanana na nguchiro wa bara la Afrika. Pamoja na fungo-bukini (nusufamilia Euplerinae) wana mhenga mmoja aliyekuwa aina ya nguchiro na aliyevuka Mlango wa Msumbiji miaka milioni 20 iliyopita[1].
Wanyama hawa ni kama nguchiro wadogo. Mdogo kuliko wote ni nguchiro-bukini miraba-myembamba (g 500) na mkubwa ni nguchiro-bukini wa Grandidier (g 1500). Rangi yao ni kahawia, kahawianyekundu au kijivu na wana miraba mwilini au mkiani isipokuwa spishi mbili za jenasi Salanoia.
Wanatokea misituni lakini nguchiro-bukini miraba-myembamba na wa Grandidier huishi katika maeneo wazi. Huchimba vishimo kama kikingio na spishi kadhaa hutumia matundu katika miti pia. Hula vertebrata wadogo, kama mijusi, vyura na wagugunaji, invertebrata kama wadudu na nge na hata matunda pengine.
Remove ads
Spishi
- Galidia elegans, Nguchiro-bukini Mkia-miraba (Ring-tailed mongoose)
- Galidictis fasciata, Nguchiro-bukini Miraba-mipana (Broad-striped Malagasy mongoose)
- Galidictis grandidieri, Nguchiro-bukini wa Grandidier (Grandidier's mongoose)
- Mungotictis decemlineata, Nguchiro-bukini Miraba-mymbamba (Narrow-striped mongoose)
- Salanoia concolor, Nguchiro-bukini Mkia-kahawia (Brown-tailed mongoose)
- Salanoia durrelli, Nguchiro-bukini wa Durrell (Durrell's vontsira)
Remove ads
Picha
- Nguchiro-bukini wa Grandidier
- Nguchiro-bukini miraba-myembamba
- Nguchiro-bukini wa Durrell
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads