Fidelis wa Sigmaringen
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Fidelis wa Sigmaringen (1578 – 24 Aprili 1622) alikuwa padri mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo, katika tawi la Wakapuchini.

Ametambuliwa na Papa Benedikto XIII kuwa mwenye heri tarehe 24 Machi 1729, halafu Papa Benedikto XIV alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini tarehe 29 Juni 1746.
Maisha
Fidelis alizaliwa katika mji wa Sigmaringen upande wa Kusini-Magharibi wa Ujerumani, mwaka 1578. Jina lake lilikuwa Mark Roy.
Alisomea Freiburg falsafa na sheria akawa wakili maarufu hasa kwa kuwatetea watu fukara.
Baadaye akajiunga na Wakapuchini, akaishi maisha magumu ya toba, makesha na sala.
Alijulikana kuwa mhubiri asiyechoka, hivyo akatumwa Uswisi hasa kwa lengo la kurudisha Waprotestanti katika Kanisa Katoliki, akawa na mafanikio makubwa hadi alipouawa na wapinzani wake mwaka 1622 mjini Seewis, akiwa anatoka katika adhimisho la Misa [2].
Ni mfiadini wa kwanza wa Idara ya Uenezaji wa Injili ya Kanisa Katoliki.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads