Fransisko Caracciolo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Fransisko Caracciolo (kwa jina la awali Ascanio Pisquizio; Villa Santa Maria, Chieti, leo katika mkoa wa Abruzzo nchini Italia, 13 Oktoba 1563 - Agnone, Isernia, mkoa wa Molise, 4 Juni 1608) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki ambaye, pamoja na Yohane Augustino Adorno, alianzisha shirika la Wakleri Watawa Wadogo, akisukumwa na upendo wake mkubwa kwa Mungu na kwa jirani.[1][2]

Fransisko alitangazwa mwenye heri na Papa Klementi XIV tarehe 4 Juni 1769, halafu mtakatifu na Papa Pius VII tarehe 24 Mei 1807.[3]
Remove ads
Maisha
Tangu ujana wake alijulikana kwa uadilifu na heshima[5].
Aliamua kutawa alipokuwa na umri wa miaka 22, kisha kupatwa na maradhi ya ngozi yaliyodhaniwa kuwa ukoma, ugonjwa usiotibika wakati huo. Hapo aliweka nadhiri ya kumtumikia Mungu na watu maisha yake yote kama atapona.
Basi, jinsi alivyopona haraka ilitafsiriwa kuwa muujiza.[6] Kwa vyovyote, alijitahidi mara moja kutimiza ahadi yake, akaenda Napoli asomee upadri.
Mwaka 1587 alipewa upadrisho akajiunga na chama cha Bianchi della Giustizia (Weupe wa Haki), ambacho lengo lake lilikuwa kuandaa waliohukumiwa kufa waweze kufa kitakatifu.
Miaka 5 baada ya kuhamia Napoli (1588) alipata kimakosa barua ya Giovanni Agostino Adorno wa Genova iliyomualika jamaa yake fulani kuungana naye katika kuanzisha shirika jipya. Fransisko aliona kosa hilo liliingia katika maongozi ya Mungu aliyemtaka yeye aitikie mwaliko huo.
Hivyo alisaidia kuandika katiba ya shirika hilo ambalo lilikubaliwa na Papa Sisto V tarehe 1 Julai 1588, likathibitishwa na Papa Gregori XIV tarehe 8 Februari 1591, tena na Papa Klementi VIII tarehe 1 Juni 1592.[5]
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads