Holmi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Holmi (Holmium) ni elementi ya kimetali yenye alama Ho na namba atomia 67, maana yake kiini cha Holmi kina protoni 67 ndani yake. Uzani atomia ni 164.930[1]. Katika jedwali la elementi inahesabiwa kati ya lanthanidi na metali za ardhi adimu.
Holmi ilitambuliwa kama elementi ya pekee nchini Uswidi na mwanakemia Per Theodor Cleve kwenye mwaka 1878. Aliikuta kama taka ndani ya oksidi ya Erbi, pamoja na Thuli. Cleve alichagua jina la Holmi kwa heshima ya mji Stockholm alikozaliwa. [2] [3] [4]
Holmi safi ni metali laini. Kiasili Holmi haipatikani kwa hali safi kwa sababu inatendana kirahisi na kemikali nyingine. Lakini inapatikana ndani ya madini monaziti na gadoliniti.[5] Maeneo makuu ya madini ni China, Marekani, Brazil, Uhindi, Sri Lanka, na Australia na akiba ya holmi inakadiriwa kuwa tani 400,000. [6]
Baada ya kusafishwa inakaa katika hewa kavu kwa halijoto ya kawaida. Ikifikia nyuzijoto °C 150 inawaka.
Holmi huwa na nguvu kubwa ya usumaku, na hapo inapita elementi zote nyingine. Kwa sababu hiyo hutumiwa kuzalisha sumaku zenye nguvu kuu. [7]
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads