Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (kwa Kiingereza: International Air Transport Association - IATA) ni umoja wa kimataifa wa kampuni za usafiri kwa ndege. Makao makuu yake yako Montreal, Quebec nchini Kanada ambako kuna pia makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa Kiraia (International Civil Aviation Organization).

IATA ilianzishwa mwaka 1945 ili kujenga ushirikiano wa makampuni makubwa ya ndege. Leo hii kuna takriban kampuni wanachama 240. Haya ni hasa makampuni ya kitaifa au makampuni makubwa ya kibiashara yanayotoa huduma za kimataifa. Mashirika madogo yanayohudumia nchi moja tu, pamoja na mashirika ya ndege za kukodi, mara nyingi si wanachama.
Kati ya kazi za IATA ni jitihada za kusanifisha tiketi za usafiri wa ndege kwa shabaha ya kuwezesha abiria kusafiri kwa mashirika mabalimbali kwa kutumia tiketi 1 tu. IATA inasaidia pia mapatano kati ya mashirika wanachama kukubaliana kati yao tiketi za makampuni mengine.
Kazi muhimu nyingine ni kutoa kodi fupi kwa kila shirika na kila uwanja wa ndege. IATA inalenga pia kusanifisha taratibu za usalama kati ya makampuni ya usafiri kwa ndege.
Remove ads
Mashirika wanachama
Mashirika yafuatayo ni wanachama wa IATA:[1]
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads