Jamhuri ya China

Nchi za Asia Mashariki From Wikipedia, the free encyclopedia

Jamhuri ya China
Remove ads

Taiwan, rasmi kama Jamhuri ya Uchina (ROC), ni nchi ya kisiwa katika Asia ya Mashariki, kilicho katika Bahari ya Pasifiki, kinachotenganishwa na Mlango wa Taiwan kutoka Jamuhuri y watu wa China. Inapakana na Uchina magharibi, Ufilipino kusini, na Japani kaskazini-mashariki. Ina idadi ya watu takriban milioni 23.5, ikiwa ya 57 duniani. Jiji lake kubwa zaidi ni New Taipei, wakati mji mkuu ni Taipei. Taiwan imegawanyika katika mikoa 22, ikijumuisha miji mikuu maalum.

Ukweli wa haraka Jamhuri ya China 中華民國, Mji mkuu ...
Remove ads

Eneo

Sehemu kubwa ya eneo lililo chini ya serikali ya Jamhuri ya China ni kisiwa cha Taiwan, lakini pia lina visiwa vidogo mbele ya mwambao wa China bara.

Mbali ya visiwa mbalimbali katika Bahari ya China visivyo na wakazi, upande wa magharibi kuna mafunguvisiwa matatu:

  • Visiwa vya Wavuvi ama Pescadores - (Penghu, 澎湖列島)
  • Quemoy (Kinmen, 金門)
  • Matsu (馬祖列島)

Historia

Jamhuri ya China iliundwa mwaka 1912 mjini Nanking baada ya mapinduzi ya China ya 1911 iliyomaliza utawala wa kifalme wa nasaba ya Qing. Sun Yat-sen akawa rais wa kwanza.

Serikali ya jamhuri ilidai mamlaka juu ya China yote ingawa hali halisi viongozi wa kijeshi na wapinzani mbalimbali walishika utawala katika maeneo kadhaa.

Nchi jinsi ilivyo sasa ni tokeo la vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China iliyokwisha mwaka 1949 na ushindi wa Wakomunisti chini ya Mao Zedong na kuundwa kwa Jamhuri ya Watu wa China huko Beijing.

Wakomunisti walifukuza serikali ya chama cha Kuomintang iliyoongoza Jamhuri ya China.

Mwaka 1949 serikali ya Kuomintang chini ya jenerali Chiang Kai-shek na mabaki ya jeshi lake pamoja na wafuasi wengi ilihamia Taiwan walipoendelea kutawala. Wakomunisti walikosa nguvu ya kuwafuata hadi kwenye visiwa kutokana na vitisho vya Marekani.

Hivyo serikali katika Taiwan iliendelea kujiita "serikali ya China" na kutangaza shabaha yake kuwa ukombozi wa China yote.

Hali halisi utawala wa Wakomunisti barani uliimarika na mipango yote kinyume chake ilionekana kama ndoto. Lakini kwa miaka minghi serikali ya Taipeh ilichukua nafasi ya China yote kimataifa.

Jamhuri ya China ilikuwa kati ya nchi zilizoanzisha Umoja wa Mataifa mwaka 1945 na serikali ya Kuomintang iliendelea kushika kiti cha China hadi mwaka 1971.

Tarehe 25 Oktoba 1971 Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliamua ya kuwa Jamhuri ya Watu wa China iwe mwakilishi wa China bara kwenye UM, hivyo Jamhuri ya China alijiondoa.

Siku hizi uhusiano kati ya China zote mbili ni mgumu. Wananchi wengi wa Jamhuri ya China wameanza kujitazama kama Wataiwani, si Wachina tena. Lakini China inadai nchi hii ni sehemu yake.

Nchi imefaulu sana kiuchumi, ikishika nafasi ya 15 duniani.

Remove ads

Watu

Wakazi ni 23,780,452 (2018), hivyo msongamano ni mkubwa sana.

Wengi wao (zaidi ya 95%) ni Wachina waliotokana na wale waliohamia kisiwani hasa kuanzia karne ya 17. Wenyeji ni 2% tu.

Kichina ndiyo lugha rasmi na ya taifa, pia lugha ya kawaida katika lahaja zake mbalimbali. Lugha za wenyeji, ambazo ni kati ya lugha za Austronesia, zinazidi kufa.

Nchi inaheshimu uhuru wa dini na wakazi wengi (81.3%) wanayo moja ya kwao. Serikali inazitambua 26.

Yenye wafuasi wengi ni Ubuddha (35.1%), Utao (33%), Ukristo (3.9%, wakiwemo Waprotestanti 2.6% na Wakatoliki 1.3%) na Yiguandao (3.5). Wenyeji wengi ni Wakristo (64%).

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads