Khanga

From Wikipedia, the free encyclopedia

Khanga
Remove ads

Khanga (au kanga) ni vazi au nguo nyepesi pia ndefu ya rangi ambayo hupendwa kuvaliwa na wanawake, hasa nchi za Afrika Mashariki na Afrika Magharibi. Kanga inafanana na kikoi ambacho kawaida huvaliwa na wanaume.

Thumb
Khanga dukani.

Kwa kawaida kanga huwa na upana wa sentimita 150 na urefu wa sentimita 110. Kanga huweza kutumiwa kama vazi rasmi, kitambaa cha kichwani, taulo, kitambaa cha mezani na kwa shughuli mbalimbali kama kubeba watoto au kubeba mizigo kichwani.

Hutumiwa pia kama zawadi kwenye sherehe za kuzaliwa, harusi, sikukuku kama vile Eid n.k.[1] Hutolewa pia kwa familia iliyofiwa na ndugu yao nchini Tanzania na hata Kenya.

Mwanzoni kanga ilikuwa ikirembwa kwa vitone vidogo ambavyo vilionekana na manyonya ya ndege aina ya kanga. Ndiyo sababu ilipewa jina hili, kwa sasa Kanga inarembeshwa kwa chapa za maua, majani na hata matunda.

Kanga huwa na sehemu tatu: pindo, mji (sehemu ya kati), na ujumbe. Ujumbe mara nyingi huwa ni kitendawili au fumbo.

Ujumbe huo kwenye kanga hutumika kupitisha ujumbe au fumbo kwa mtu, mfano mke kwa mumewe au swahiba kwa swahibae au kwa swahiba/marafiki, ujumbe unaweza kuwa kwa nia ya kumshukuru, kumkanya, kutoa hongera au kwa ajili ya mapenzi.

Hii ni mifano ya ujumbe wa kwenye kanga.

  • Majivuno hayafaif[2]
  • Mkipendana mambo huwa sawa
  • Japo sipati tamaa sikati [2]
  • Wazazi ni dhahabu kuwatunza ni thawabu: [2]
  • Sisi sote abiria dereva ni Mungu[2]
  • Fimbo la mnyonge halina nguvu[3]
  • Mwanamke mazingira tunataka, usawa, amani, maendeleo[2]
  • Naogopa simba na meno yake siogopi mtu kwa maneno yake[2].
  • Leo ni siku ya shangwe na vigelegele
  • Subira huvuta kheri.
  • Wawili wakipenda adui hana nafasi.
  • Hakuna kama mama.
Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads