Lambo la Kihansi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Lambo la Kihansi linapatikana nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro na linaunda bwawa la maji ya mto Kilombero litumikalo kuzalisha umeme kwa njia ya kani mvutano yaani graviti.
Bwawa la Kihansi lina uwezo wa kuzalisha hadi megawatts 180 (241,384 hp) ambapo linachangia asilimia 13 ya umeme unaozalishwa nchini Tanzania [1].
Remove ads
Mahali
Bwawa la Kihansi, ambalo limetokana na lambo hilo, linapatikana kusini mwa Tanzania kukatisha mto Kilombero katika korongo la Kihansi baada ya kukutana na mto ulanga. Kutoka Dar es Salaam inakadiriwa kuwa kilometa 643 kusini[2], wakati kutoka Iringa inakadiriwa ni kilometa 168 kusini, mpakani mwa Wilaya ya Mufindi na Wilaya ya Kilombero[3].
Historia
Bwawa la Kihansi linamilikiwa na shirika la umeme la Tanzania TANESCO. Lilianza kujengwa mnamo Julai 1995 likakamilika na kisha kufunguliwa na Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin W. Mkapa tarehe 10 Julai 2000.
Ujenzi wake uligharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni 275 [1][4].
Marejeo
Tazama pia
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads