Kismayu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kismayu (pia: Kismayo au kwa Kisomali: Kismaayo) ni mji katika mkoa wa Jubbada Hoose wa Somalia mwambaoni mwa Bahari Hindi. Uko karibu na mdomo wa mto Juba. Kismayu ndio mji mkubwa katika eneo la Jubbaland. Mji wenyewe uko km 528 kusini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.


Katika mwaka wa 2011, Kismayu ilikadiriwa kuwa na wakaazi 183,300[1].
Remove ads
Historia
Mji ulianzishwa na Wabajuni waliokuwa Waswahili Wabantu. Wasomali wenyewe walichelewa kufika eneo hili. Katika karne za kati, Kismayu ilikuwa chini ya serikali ya Ajuuraan iliyokuwa ikutawala eneo kadhaa za Somalia.
Kismayu pamoja na pwani ilikuwa chini ya masultani wa Zanzibar tangu 1835 BK. Kati ya 1875 na 1876 Kismayu ilitawaliwa na Misri.
Tangu 1895 ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza pamoja na Kenya lakini mwaka 1924 ilikabidhiwa kwa utawala wa Italia. Ikawa mji mkuu wa jimbo la Oltre Giuba (ng'ambo ya Juba).
Kismayu iliharibika sana kutokana na mapigano katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Somalia tangu 1991.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads